JARIDA LA UGHAIBUNI

Thursday, February 23, 2006

LUBUVA AHUTUBIA MENLO PARK ROTARY

Ndugu wasomaji jana ilikuwa siku ya pekee kwangu kuintangaza nchi yangu pale nilipopewea nafasi ya kuihutubia Rotary Klab ya Menlo Park hapa California. Niliongea Juu biashara huria na nafasi za uwekezaji nchini Tanzania. Baadhi ya mambo niliyoongelea ni Sekta muhimu za mawasiliano, miundombinu, usafiri wa majini na nchi kavu, mabenki na taasisi za bima, madini na taasisi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na mambo ya kijamii na uchumi.

Mazungunzo yalihusisha nafasi za uwekezaji kama vile uwekezaji katika madaraja na barabara, ununuzi wa hisa za benki ya NMB, usafiri wa boti ziendazo kasi na mambo mengine mengi. Wasikilizaji wenye msimamo wa Kikonservative walivutiwa sana na kuuliza maswali mengi yenye mwelekeo wa nia ya uwekezaji. Mmoja wao alitoa pendekezo la kuanziasha taasisi ya mikopo midogo midogo nchini Tanzania.

Sunday, February 05, 2006

KENYA IMEOZA KWA UFISADI


Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako. Usemi huu umedhihirika hivi majuzihuko nchini kenya ambako Serikali ya mwai kibaki imepata kashfa ya kula mamilioni ya pesa ya walipa kodi ya Kenya. Maafisa wa ngazi za juu wa Serikali hiyo, wamegundua namna ya kula pesa pesa kwa staili ya kisasa kwa kutengeneza makampuni hewa Kama ya Anglo Leasing. Kulia ni Raisi Mwai Kibaki wa Kenya anyeoongoza serikali iliyooza kwa ufisadi

Wakati kashfa ya Anglo leasing ikiunguruma, kahfa nyingine mpya imezuka, pale Raisi mwai kibaki alipokabidhiwa rundo la kesi za ufisadi mapema mwaka jana, na Balozi wa Uingereza nchini humo bw. Edward Clay, na kuzitupilia mbali. Siri imbayo imejitokeza ni kuwa katika kashfa hizo, viongozi wa serikali wamehusika kwa kuwekeza katika makampuni kwa kuficha utambulishi wao .
Kilicho nivutia zaidi ni pale kampuni ya simu za mkononi inayoongozwa na mwalimu mwezangu wa kiswahili hapa Stanford University Dr. Angaluki Muaka aliponyonyimwa leseni ya kufanya kazi nchini Kenya. Kampuni hiyo ilinyimwa kibali cha Usajili kwa sababu ingekuwa tishio kwa vijikampuni vilivyo sajiliwa kwa mgongo wa vigogo na kendeshwa na pesa za walipa kodi zilizoibiwa na vigogo hao. Kesi ya kampuni hiyo kunyimwa leseni inaunguruma hadi sasa nchini kenya. Hivi sasa, Dr. Angaluki Muaka na wenzake, wamepata kibali kingine cha kundesha kampuni ya simu za "landline" iitwayo Sasatel. Bonyeza hapa http://www.eastandard.net/hm_news/news.php?articleid=35965 upate uhondo wa skendo hilo nchini Kenya.

Thursday, February 02, 2006

UJAMBAZI DAR WATISHIA AMANI


Katika hali ya kukatisha tamaa, majambazi yamepora mamilioni ya shilingi, jana saa tatu na nusu asubuhi katika benki ya NBC Ubungo Dar es Salaam. Hili ni tukio moja tu kati ya mfululizo wa matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yaliotokea miezi sita iliyopita.Alfred Tibaigana Kamanda wa Polisi anayeshindwa
Kudhibiti wimbi la Ujambazi Dar. Source IPP Media


Chakujiuliza, serikali kupitia jeshi lake la polisi wanafanya nini kulinda usalama wa raia na mali zao? Mbona jeshi la polisi limepoa kama nyama ya kondoo tena iliyowekwa kwenye friji? Chakushangaza katika tukio la ujambazi la NBC Ubungo majambazi
yamepora asubuhi kweupeee, tena katika eneo lenye msongamno mkubwa wa watu (Ubungo stendi) na

Hii inamaanisha majambazi hayo yalikuwa na uhakika wa usalama wao. Kutokana na duru za mashuhuda wa tukio hilo, majambazi hayo yametoka na mabegi yaliyobeba mamilioni ya pesa na yameondoka katika staili ya mwendo wa kinyonga. Swali la kujiuliza jeshi la polisi lilikuwa wapi muda wote? Kwa nchi yenye jeshi lijishuhulishalo silingekamata majambazi hayo?.

Kama vile majambazi hayo yamefadhililiwa na idara hiyo njeti usalama nchini, Kamanda wa polisi mkoa wa Dar es Salaam alipopigiwa simu na Alfred Tibaigana na mmoja wa wateja alimjibu kuwa, anataarifa ya ujambazi huo. Chakushangaza kwa nini hakutuma jeshi lake la polisi mara moja kudhibiti ujambazi huo? Hali hii inakatisha tamaa katika Tanzania bila nyerere.

Kushindwa huku kwa jeshi la polisi kudhibiti wimbi la ujambazi, kunadhihirisha umuhimu wa kufanya mabadiliko njeti katika idara hiyo, ukiwemo ung'atukaji wa wa baadhi ya maofisa wa ngazi za juu za idara hiyo kwa kushindwa kufanya kazi. La sivyo, hizo ahadi za jeshi la Ulinzi na Kugenga taifa kudhibiti wimbi hilo la ujambazi zitimilizwe. Inaniuma sana pale raia waliochuma mali zao kwa jasho lao, kuzipoteza kwa raia wanaodai mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe. Inauma zaidi pale raia wema wanapopoteza maisha yao kupigwa risasi hadi kufa wakati wa uporaji kama nilivyoshuhudia mam lishe alipopigwa risasi hadi ubongo nje nyuma ya Maziwa Guest House Ububgo,August mwaka jana.

Chanzo cha Ujambazi

Hakuna mtu apendaye kuwa jambzazi ila mzazingira ya kiuchumi yaliyopo ncini yanaweza changia kwa kiasi kikubwa sana kuzuka wimbi la ujambazi. Nidhahiri kuwa vijana wengi sana Tanzania hawajaajiriwa. Hivyo ni rahisi kwao kujiingiza katika ujambazi. Mbali ya kukosa ajira, mishahara walipwayo watanzania ni midogo mno. Hii ndiyo maana baadhi ya wafanyakazi katika vyombo vya usalama walipwao mishahara midogo hujihusha katika ujambazi wa kutumia silaha. Imefika wakati watanzania tupandishe mishahara na kima cha chini kufikia walao Tsh 300,000. Hii inawezekana kama mishahara itaongezwa na kodi kuongezwa ili serikali ijipatie pesa za kuwalipa wafanyakazi wake na kuendesha shughuli zake kama ilivyo nchi zilizoendelea kama Marekani. Ni aibu kusikia baamedi wa Marekani akitengeneza pesa mara tano ya profesa wa chuo kikuu Tanzania kwa mwezi

Umilikaji wa silaha kwa watu binafsi na kuanzishwa kwa makampuni binafsi ya ulinzi kumechangia kuzagaa kwa silaha nchini. Hii ni kutokana na kuiga staili za maisha ya wenzetu mamtoni, bila ya kuandaa mazingira ya kumudu staili hizo za maisha. Matokeo yake silaha hizo zinatumika kuwaliza watanzania. Haya Baba Kikwete uliyeahidi ajira kwa vijana na kuberesha maisha ya watanzania, kazi kwako, mbona majambazi yanakutingishia kiberiti na hatujaona makali yako?

Tuesday, January 31, 2006

KARIBU JARIDA LA UGHAIBUNI


Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako. Usemi huu umedhihirika hivi majuzihuko nchini kenya ambako Serikali ya mwai kibaki imepata kashfa ya kula mamilioni ya pesa ya walipa kodi ya Kenya. Maafisa wa ngazi za juu wa Serikali hiyo, wamegundua namna ya kula pesa pesa kwa staili ya kisasa kwa kutengeneza makampuni hewa Kama ya Anglo Leasing. Kulia ni Raisi Mwai Kibaki, anayeongoza serikali iliyooza kwa Ufisadi

Wakati kashfa ya Anglo leasing ikiunguruma, kahfa nyingine mpya imezuka, pale Raisi mwai kibaki alipokabidhiwa rundo la kesi za ufisadi mapema mwaka jana, na Balozi wa Uingereza nchini humo bw. Edward Clay, na kuzitupilia mbali. Siri imbayo imejitokeza ni kuwa katika kashfa hizo, viongozi wa serikali wamehusika kwa kuwekeza katika makampuni kwa kuficha utambulishi wao .
Kilicho nivutia zaidi ni pale kampuni ya simu za mkononi inayoongozwa na mwalimu mwezangu wa kiswahili hapa Stanford University Dr. Angaluki Muaka aliponyonyimwa leseni ya kufanya kazi nchini Kenya. Kampuni hiyo ilinyimwa kibali cha Usajili kwa sababu ingekuwa tishio kwa vijikampuni vilivyo sajiliwa kwa mgongo wa vigogo na kendeshwa na pesa za walipa kodi zilizoibiwa na vigogo hao. Kesi ya kampuni hiyo kunyimwa leseni inaunguruma hadi sasa nchini kenya. Hivi sasa, Dr. Angaluki Muaka na wenzake, wamepata kibali kingine cha kundesha kampuni ya simu za "landline" iitwayo Sasatel. Bonyeza hapa http://www.eastandard.net/hm_news/news.php?articleid=35965 upate uhondo wa skendo hilo nchini Kenya.