JARIDA LA UGHAIBUNI

Thursday, February 02, 2006

UJAMBAZI DAR WATISHIA AMANI


Katika hali ya kukatisha tamaa, majambazi yamepora mamilioni ya shilingi, jana saa tatu na nusu asubuhi katika benki ya NBC Ubungo Dar es Salaam. Hili ni tukio moja tu kati ya mfululizo wa matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yaliotokea miezi sita iliyopita.Alfred Tibaigana Kamanda wa Polisi anayeshindwa
Kudhibiti wimbi la Ujambazi Dar. Source IPP Media


Chakujiuliza, serikali kupitia jeshi lake la polisi wanafanya nini kulinda usalama wa raia na mali zao? Mbona jeshi la polisi limepoa kama nyama ya kondoo tena iliyowekwa kwenye friji? Chakushangaza katika tukio la ujambazi la NBC Ubungo majambazi
yamepora asubuhi kweupeee, tena katika eneo lenye msongamno mkubwa wa watu (Ubungo stendi) na

Hii inamaanisha majambazi hayo yalikuwa na uhakika wa usalama wao. Kutokana na duru za mashuhuda wa tukio hilo, majambazi hayo yametoka na mabegi yaliyobeba mamilioni ya pesa na yameondoka katika staili ya mwendo wa kinyonga. Swali la kujiuliza jeshi la polisi lilikuwa wapi muda wote? Kwa nchi yenye jeshi lijishuhulishalo silingekamata majambazi hayo?.

Kama vile majambazi hayo yamefadhililiwa na idara hiyo njeti usalama nchini, Kamanda wa polisi mkoa wa Dar es Salaam alipopigiwa simu na Alfred Tibaigana na mmoja wa wateja alimjibu kuwa, anataarifa ya ujambazi huo. Chakushangaza kwa nini hakutuma jeshi lake la polisi mara moja kudhibiti ujambazi huo? Hali hii inakatisha tamaa katika Tanzania bila nyerere.

Kushindwa huku kwa jeshi la polisi kudhibiti wimbi la ujambazi, kunadhihirisha umuhimu wa kufanya mabadiliko njeti katika idara hiyo, ukiwemo ung'atukaji wa wa baadhi ya maofisa wa ngazi za juu za idara hiyo kwa kushindwa kufanya kazi. La sivyo, hizo ahadi za jeshi la Ulinzi na Kugenga taifa kudhibiti wimbi hilo la ujambazi zitimilizwe. Inaniuma sana pale raia waliochuma mali zao kwa jasho lao, kuzipoteza kwa raia wanaodai mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe. Inauma zaidi pale raia wema wanapopoteza maisha yao kupigwa risasi hadi kufa wakati wa uporaji kama nilivyoshuhudia mam lishe alipopigwa risasi hadi ubongo nje nyuma ya Maziwa Guest House Ububgo,August mwaka jana.

Chanzo cha Ujambazi

Hakuna mtu apendaye kuwa jambzazi ila mzazingira ya kiuchumi yaliyopo ncini yanaweza changia kwa kiasi kikubwa sana kuzuka wimbi la ujambazi. Nidhahiri kuwa vijana wengi sana Tanzania hawajaajiriwa. Hivyo ni rahisi kwao kujiingiza katika ujambazi. Mbali ya kukosa ajira, mishahara walipwayo watanzania ni midogo mno. Hii ndiyo maana baadhi ya wafanyakazi katika vyombo vya usalama walipwao mishahara midogo hujihusha katika ujambazi wa kutumia silaha. Imefika wakati watanzania tupandishe mishahara na kima cha chini kufikia walao Tsh 300,000. Hii inawezekana kama mishahara itaongezwa na kodi kuongezwa ili serikali ijipatie pesa za kuwalipa wafanyakazi wake na kuendesha shughuli zake kama ilivyo nchi zilizoendelea kama Marekani. Ni aibu kusikia baamedi wa Marekani akitengeneza pesa mara tano ya profesa wa chuo kikuu Tanzania kwa mwezi

Umilikaji wa silaha kwa watu binafsi na kuanzishwa kwa makampuni binafsi ya ulinzi kumechangia kuzagaa kwa silaha nchini. Hii ni kutokana na kuiga staili za maisha ya wenzetu mamtoni, bila ya kuandaa mazingira ya kumudu staili hizo za maisha. Matokeo yake silaha hizo zinatumika kuwaliza watanzania. Haya Baba Kikwete uliyeahidi ajira kwa vijana na kuberesha maisha ya watanzania, kazi kwako, mbona majambazi yanakutingishia kiberiti na hatujaona makali yako?

9 Comments:

At 2:37 AM, Blogger mwandani said...

Macho ya huyo askari kwenye picha tisha toto tu, majambazi wanamzunguka hafanyi lolote. Wakimkamata pikpoket, raia watamtia ngeu, manjagu watampa kibano, upande wa pili majambazi wanachukua vyao taratiibu. Tanzania tunaenda wapi?

 
At 5:38 AM, Blogger January John said...

Heheee!!!Huyu Tibaigana arudi Bukoba tu aache kutowa macho kama vile amepandisha hoka.Majambazi hawa wanatakiwa washughulikiwa na siyo zogo la ofsini tu.Tangu lini ujambazi ukashughulikiwa kupitia vyombo vya habari?Nashukuru kijana wangu wa jarida la ughaibuni japokuwa uko kwa Shwaziniga, inabidi uwafunulia hayo mawazo yako hao wadanganyika ili wazinusuru roho za wenzetu na mali zao.

 
At 9:19 AM, Blogger boniphace said...

Macho ya wizi hayo yaani alikuwa hajui kuwa kuna kamisheni ya kila tukio la wizi hapo Dar. Ngoja waendelee kumaliza umma walioahidi kuulinda. Haya ndiyo madhara ya kutothamini viapo.

 
At 11:57 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Macho hayo anatumia "lile jani" nini?

 
At 2:11 PM, Blogger John Mwaipopo said...

Kati ya vitu vinavyopandisha hofu yangu pale nitakaporejea Da'slam ni ujambazi. Yaani kweli jeshi la polisi limeshindwa kudhibiti tujambazi tuchace tu. Nadiliki kusema tuchache kwani kwa kawaida Bongo majambazi wanaohusika katika matukio mbalimbali ni wale wale tu

 
At 8:01 AM, Blogger Indya Nkya said...

Majambazi Tanzania wanaweza kuwa wawili au watatu tuu. Wengine ni waajiriwa. Uzuri ni kwamba polisi wanawajua ila hawataki kuwakamata kwa vile kama laivyosema Makene kila tukio la ujambazi linalotokea kuna asilimia kumi!!

 
At 8:57 AM, Blogger zarena kewat said...

That's what everyone likes. You have a good imagination. Great post thanks you
vimax canada

 
At 9:06 PM, Blogger yanmaneee said...

valentino
harden shoes
nike air force
hermes
adidas gazelle
off white
nike basketball shoes
off white clothing
timberland boots
vapormax

 
At 2:56 AM, Blogger myslot said...

แนะนำเลยครับหนังออนไลน์ Captain Marvel กัปตัน มาร์เวล (2019) หนังใหม่ดูเมื่อไหร่ก็ฟรี

https://www.doonung1234.com/

 

Post a Comment

<< Home