JARIDA LA UGHAIBUNI

Tuesday, January 31, 2006

KARIBU JARIDA LA UGHAIBUNI


Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako. Usemi huu umedhihirika hivi majuzihuko nchini kenya ambako Serikali ya mwai kibaki imepata kashfa ya kula mamilioni ya pesa ya walipa kodi ya Kenya. Maafisa wa ngazi za juu wa Serikali hiyo, wamegundua namna ya kula pesa pesa kwa staili ya kisasa kwa kutengeneza makampuni hewa Kama ya Anglo Leasing. Kulia ni Raisi Mwai Kibaki, anayeongoza serikali iliyooza kwa Ufisadi

Wakati kashfa ya Anglo leasing ikiunguruma, kahfa nyingine mpya imezuka, pale Raisi mwai kibaki alipokabidhiwa rundo la kesi za ufisadi mapema mwaka jana, na Balozi wa Uingereza nchini humo bw. Edward Clay, na kuzitupilia mbali. Siri imbayo imejitokeza ni kuwa katika kashfa hizo, viongozi wa serikali wamehusika kwa kuwekeza katika makampuni kwa kuficha utambulishi wao .
Kilicho nivutia zaidi ni pale kampuni ya simu za mkononi inayoongozwa na mwalimu mwezangu wa kiswahili hapa Stanford University Dr. Angaluki Muaka aliponyonyimwa leseni ya kufanya kazi nchini Kenya. Kampuni hiyo ilinyimwa kibali cha Usajili kwa sababu ingekuwa tishio kwa vijikampuni vilivyo sajiliwa kwa mgongo wa vigogo na kendeshwa na pesa za walipa kodi zilizoibiwa na vigogo hao. Kesi ya kampuni hiyo kunyimwa leseni inaunguruma hadi sasa nchini kenya. Hivi sasa, Dr. Angaluki Muaka na wenzake, wamepata kibali kingine cha kundesha kampuni ya simu za "landline" iitwayo Sasatel. Bonyeza hapa http://www.eastandard.net/hm_news/news.php?articleid=35965 upate uhondo wa skendo hilo nchini Kenya.

10 Comments:

At 9:58 AM, Blogger boniphace said...

Karibu sana Jacob, nadhani nimeshapita kwangu na kukuiweka ili wasomaji wangu wakufikie kukupa salamu. Naona mwanzo huu ni mwema na kumbuka kutuwekea habari ulizoahidi jana usiku maana tunazisubiri kwa hamu. Pia safi sana kutangaza Blogu kuwa haki za kila raia Tanzania.

 
At 12:11 PM, Blogger John Mwaipopo said...

Karibu mwana kwetu Jacob Lubuva. Tumekuwa tukikusubiri kwa hamu sana na hatimaye kiu yetu sasa imekatika. Sasa tuna uhakika wa kupaata yanayojiri huko California na kwingineko. Sikuwa najua kuwa kuwa na blogu ni haki ya msingi ya kila mtanzania . Kweli umetoka kivyako.

 
At 4:50 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Lubuva,
Karibu sana.Jisikie upo huru zaidi.Uhuru wa kusema ukasikika ni uhuru mzuri sana.Maendekeo huanza na kusemezana,kuelimishana,kukosoana na bila kusahau kusifiana inapostahili.Karibu sana uwanjani.

 
At 10:09 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Lubuva,
Tunafurahi sana sana kupata habari hizi njema za kuzaliwa kwa mwanablogu mpya na juhudi za Makene. Karibu sana. Tunayofanya leo kupitia blogu zetu ni msingi wa mapinduzi makubwa yanayosambaa duniani kutokana na teknolojia mpya za habari na mawasiliano. Ingawa kwetu bado watu wachache wanatumia mtandao wa tarakilishi, wale ambao tuna uwezo wa kutumia tuna kila sababu ya kutengeneza njia.

 
At 2:01 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

karibu sana bwana lubuva...ni vyema sana kukohoa kwani huwezi ishi na kikohozi....amini usiamini kohozi lako ndio dawa ya matatizo...karibu sana

 
At 3:50 AM, Blogger Innocent Kasyate said...

Bwana Lubuva karibu sana na ninakuhakikishia hutajuta uamuzi wako wa kuwa mwanaglobu.
Wewe utatulete ya ughaibuni ila sisi tutakupa ya uswazi.

 
At 9:12 AM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Karibu sana kaka!
Ninacofanya saa hivi ni kuweza kuwahakikishia kuwa wtzanainia wenzangu kuwa blogu ni haki ya kila mtanzania.Hii teknolojia ya blogui wate wengi wamekuwa haiielewi.Wengi wo niliokuw nikiwashawishi kuwa blogu zao kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika jamii wanayoishi wamekuwa wagumu kukubali kuwa njia hii ni haki ya kila raia.Nimekuwa nikipata kazi hasa kwa wanavyuo.
lazima tuutoe huu "utando" katika vichwa vya WATZ.

 
At 1:52 AM, Blogger Indya Nkya said...

Nilichelewa kukukaribisha. Karibu ndugu yangu tuwemo wote

 
At 9:00 AM, Blogger zarena kewat said...

That's what everyone likes. You have a good imagination. Great post thanks you
vimax canada

 
At 9:06 PM, Blogger yanmaneee said...

air force 1
balenciaga
russell westbrook shoes
ferragamo belt
yeezy boost
moncler outlet
yeezy boost 350
goyard
coach factory outlet
kyrie 6 shoes

 

Post a Comment

<< Home