JARIDA LA UGHAIBUNI

Tuesday, January 31, 2006

KARIBU JARIDA LA UGHAIBUNI


Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako. Usemi huu umedhihirika hivi majuzihuko nchini kenya ambako Serikali ya mwai kibaki imepata kashfa ya kula mamilioni ya pesa ya walipa kodi ya Kenya. Maafisa wa ngazi za juu wa Serikali hiyo, wamegundua namna ya kula pesa pesa kwa staili ya kisasa kwa kutengeneza makampuni hewa Kama ya Anglo Leasing. Kulia ni Raisi Mwai Kibaki, anayeongoza serikali iliyooza kwa Ufisadi

Wakati kashfa ya Anglo leasing ikiunguruma, kahfa nyingine mpya imezuka, pale Raisi mwai kibaki alipokabidhiwa rundo la kesi za ufisadi mapema mwaka jana, na Balozi wa Uingereza nchini humo bw. Edward Clay, na kuzitupilia mbali. Siri imbayo imejitokeza ni kuwa katika kashfa hizo, viongozi wa serikali wamehusika kwa kuwekeza katika makampuni kwa kuficha utambulishi wao .
Kilicho nivutia zaidi ni pale kampuni ya simu za mkononi inayoongozwa na mwalimu mwezangu wa kiswahili hapa Stanford University Dr. Angaluki Muaka aliponyonyimwa leseni ya kufanya kazi nchini Kenya. Kampuni hiyo ilinyimwa kibali cha Usajili kwa sababu ingekuwa tishio kwa vijikampuni vilivyo sajiliwa kwa mgongo wa vigogo na kendeshwa na pesa za walipa kodi zilizoibiwa na vigogo hao. Kesi ya kampuni hiyo kunyimwa leseni inaunguruma hadi sasa nchini kenya. Hivi sasa, Dr. Angaluki Muaka na wenzake, wamepata kibali kingine cha kundesha kampuni ya simu za "landline" iitwayo Sasatel. Bonyeza hapa http://www.eastandard.net/hm_news/news.php?articleid=35965 upate uhondo wa skendo hilo nchini Kenya.